TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Saturday, July 16, 2016

SHEVCHEKO ATEULIWA KUWA MENAJA WA UKRAINE

Ukraine imemteua mshambuliaji wa zamani wa AC Milan na Chelsea Andriy Shevchenko kuwa meneja mpya wa timu ya taifa.

Shevchenko, 39, aliyechezea timu ya taifa mara 111, atajaza nafasi ya Mykhaylo Fomenko, aliyeondoka baada ya taifa hilo kuondolewa michuano ya Euro 2016 katika hatua ya makundi.

Shevchenko alikuwa msaidizi wa Fomenko Ukraine waliposhindwa mechi zao zote dhidi ya Ujerumani, Ireland Kaskazini na Poland.

Mchezaji huyo wa zamani wa Dynamo Kyiv, aliyestaafu mwaka 2012, hajawahi kuhudumu kama meneja awali.


Ukraine's record scorer with 48 goals, Shevchenko ndiye anayeshikilia rekodi ya ufungaji mabao timu ya taifa ya Ukraine na alikuwa nahodha walipofuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2006.

Ametia saini mkataba wa miaka miwili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: SHEVCHEKO ATEULIWA KUWA MENAJA WA UKRAINE Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA