TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Monday, July 25, 2016

ZITTO KABWE AALIKWA MAREKANI

Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe ameondoka Nchini kuelekea Philadelphia Nchini Marekani Kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention) utakaomthibitisha Bi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais kupitia Chama hicho.

Wakati Akiwa kwenye Mkutano huo Ndugu Zitto atapata Fursa ya Kufanya Mazungumzo Na Viongozi mbalimbali wa Kisiasa duniani, Kufanya Kikao Cha Maandalizi Juu ya Ufunguzi wa Tawi la Wanachama wa ACT Diaspora la Nchini Marekani pamoja na Kuwa Na Mazungumzo Maalum na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad Juu ya Hali ya Kisiasa ya Zanzibar na Taifa Kwa Ujumla. Zitto na Maalim Seif ndio wanasiasa pekee nchini walioalikwa kwenye shughuli za chaguzi za nchini Marekani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: ZITTO KABWE AALIKWA MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA