TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Monday, August 29, 2016

MAKABIDHIANO YA OFISI MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA- NIDA

 Dr. Modestus Kipilimba (Kushoto) akimkabidhi ripoti ya utekelezaji mradi wa vitambulisho vya Taifa Bw. Andrew Wilson Massawe aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA wakati wa hafla ya Makabidhiano katika ofisi za  Makao makuu ya NIDA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Bw. Andrew Wilson Massawe akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa mara baada ya hafla ya makabidhiano.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dr. Modestus Kipilimba aliketi kushoto na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew Wilson Massawe wakiwa katika  picha ya pamoja na Menejimenti ya NIDA, baada ya hafla fupi ya makabidhiano.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Bw. Andrew Wilson Massawe akikagua mitambo ya uzalishaji vitambulisho alipotembea kituo cha uchakataji na uzalishaji vitambulisho mara baada ya halfa ya makabidhiano. Kulia ni aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa akishuhudia.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, akikagua mfumo wa uhifadhi taarifa wakati alipotembelea kituo cha uchakataji taarifa (Data Centre) na kushuhudia mfumo wa kielektroniki unavyoendesha shughuli mbalimbali za uzalishaji na uhifadhi wa taarifa katika kituo hicho.

Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dr. Modestus Kipilimba akifafanua jambo wakati akihitimisha ziara ya makabidhiano katika kituo cha uchakataji na uzalishaji vitambulisho. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Bw. Andrew Wilson Massawe akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti,
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MAKABIDHIANO YA OFISI MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA- NIDA Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA