TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Thursday, September 15, 2016

UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA KWA WAHESHIMIWA WABUNGE -DODOMA

 Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa jimbo la Musoma, Mhe.Profesa Sospeter Muhongo akipokea Kitembulisho chake cha Taifa chenye saini kwa furaha kubwa kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Na Hifadhi Hati NIDA. Bi. Rose Mdami.

Mheshimiwa Waziri wa Katiba na na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe, akiwa mwenye furaha kubwa baada ya kuchukua Kitambulisho chake kipya Bungeni Dodoma. NIDA imeanza kutoa vitambulisho vipya vyenye saini kwa viongozi wakiwemo Waheshimiwa Wabunge zoezi linaloedelea mkoani Dodoma sambamba na kikao cha Bunge.

Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mheshimiwa Andrew Chenge akisilikiliza kwa makini maelezo kuhusu Kitambulisho Kipya cha Taifa kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati NIDA Bi. Rose Mdami Bungeni Dodoma alipofika kuchukua kitambulisho chake mapema leo.

Mbunge wa Vita Maalum Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Dr. Elly Macha akipokea kwa furaha Kitambulisho chake kipya chenye saini kutoka kwa Afisa Usajili Wilaya ya Dodoma Mjini Bwana Khalid Mrisho.

Mheshimiwa Deo Sanga, akieleza faida ambazo tayari ameshazipata kwa kutumia Kitambulisho chake cha Taifa. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi hati NIDA Bi, Rose Mdami. Mhe. Sanga amepokea kitambulisho chake leo katika Ofisi za Bunge Dodoma.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipata huduma kutoka kwa maafisa wa NIDA ambao wapo bungeni hapo kutoa vitambulisho vipya kwa waheshimiwa wabunge Mjini Dodoma.

Mbunge wa Muheza na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Bunge Mheshimiwa Adadi Rajabu akipokea kitambulisho chake kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati NIDA Bi. Rose Mdami katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA KWA WAHESHIMIWA WABUNGE -DODOMA Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA