TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Tuesday, November 15, 2016

TB Joshua arejesha utabiri wa ushindi wa Clinton Facebook

Utabiri kutoka kwa mhubiri raia wa Nigeria TB Joshua kuwa Hillary Clinton angeshinda urais wa Marekani, umerejeshwa tena baada ujumbe huo kufutwa kutoka mtandao wa Facebook.

Kulingana na barua pepe iliyotumwa kwa BBC na idara ya mitandao ya kanisa la TBJMinistries ilisema kuwa , "ujumbe huo uliondolewa kimakosa na sasa umerejeshwa kwa kuwa hiyo si sera yetu."

"Siku kumi zilizopita nilimuona rais wa Marekania akishinda kwa kura chache, yule niliyemuona ni mwanamke," ujumbe huo ulisema.

TB Joshua alikejeliwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii wakati watu walitambua kuwa ujumbe huo ulikuwa umefutwa, licha ya wafuasi wake wengi katika mitandao ya kijamii bado kumtaja kuwa nabii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: TB Joshua arejesha utabiri wa ushindi wa Clinton Facebook Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA